Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kama kupiga kura ni miaka 18 kwa nini isiwe katika ubunge? -Seneta:Kilonzo

Kama kupiga kura ni miaka 18 kwa nini isiwe katika ubunge? -Seneta:Kilonzo

Iwapo sheria inaruhusu mtu kupiga kura akiwa na umri wa miaka 18, basi mtu huyo anapaswa pia kuwa na uwezo wa kuwakilisha watu bungeni ili kuweza kushiriki katika uamuzi na hivyo kufanikisha ajenda 2030.

Hiyo ni kauli ya Seneta wa kaunti ya Makueni kutoka Kenya, Mutula Kilonzo Jr. akiwakilisha nchi yake kwenye mkutano kuhusu wabunge vijana unaofanyika mjini Lusaka Zambia.

Katika mahojiano maalum na Idhaa hii Bwana Kilonzo amesema ni muhimu vijana wakashirikishwa katika nafasi hizo huku akitolea mfano nchi yake

(Sauti ya Kilonzo)

Kuhusu taswira ya uwakilishi kati ya wanawake na wanaume vijana kwenye bunge la Kenya,  amesema…

(Sauti)

Mkutano huo wa siku mbili unaomalizika leo unalenga kuchagiza ushirikishaji wa vijana katika bunge ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu kwa kuhusisha vijana katika uamuzi.