Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumaini kwa wanawake na wasichana laangaziwa katika CSW60

Tumaini kwa wanawake na wasichana laangaziwa katika CSW60

Matukio mbalimbali ya mkutano wa 60 wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW60 yanaendelea, ambapo mada kuhusu tumaini kwa wanawake na wasichana kutoka katika madhila imeghubika mjadala, katika tukio lililoandaliwa na mashirika ya kiraia yenye uhusiano na idara ya Umoja wa Mataifa ya mawasiliano kwa umma, DPI. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(TAARIFA YA MMALI)

Mkutano huo umeibua hisia za wanawake na wasichana waliopitia dhoruba kadhaa katika kujikomboa na kilichowagusa wengi ni ujumbe kwa njia ya video kutoka kwa mtoto Malala Yusufzai ambaye alipigwa risasi na wanamgambo nchini Pakistan ili kumzuia kutimizia malengo ya elimu kwa wasichana.

Na kisha hadhira hiyo ikasilikiza ushuhuda wa manusura wa mauaji ya kimbari ya Rwanda Consolee Nishimwe ambaye aliwahamasisha wanawake kuwa licha ya magumu ya ukandamizaji wanayoweza kupitia kama kubakwa kitendo kilichomkumba yeye,  bado wanaweza kuibuka katika matumaini.

( SAUTI CONSOLEE)

Wanawake na wasichana mbalimbali wanaowakilisha asasi tofauti walielezea namna walivyochomoza kutoka katika ukandamizaji unaotokana na vita na mila potofu.