Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atoa heko kwa rais mpya wa Myanmar

Ban atoa heko kwa rais mpya wa Myanmar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametuma risala za pongezi kwa rais mpya wa Myanmar, U Htin Kyaw, ambaye alichaguliwa na bunge la nchi hiyo kama rais wa kwanza wa kiraia wa Jamhuri ya Muungano ya Myanmar katika kipindi cha zaidi ya miongo mitano.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imesema Ban amekaribisha tukio hilo kama hatua ya ufanisi katika kuendeleza mabadiliko ya kidemokrasia yaliyowekwa na serikali inayoondoka.

Aidha, Katibu Mkuu ameelezea matumaini yake kuwa watu wa Myanmar wataendelea kwa subira kwa njia ya demokrasia na maridhiano ya kitaifa, na kutoa wito kwa rais mteule, U Htin Kyaw, na kwa wadau wengine wote, kufanya kazi pamoja ili kuimarisha umoja na ustawi wa nchi hiyo kwa amani.