Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU yachangia WFP kwa ajili ya wakimbizi wa Syria

EU yachangia WFP kwa ajili ya wakimbizi wa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP limekaribisha leo mchango wa dola milioni 43 uliotolewa na Muungano wa Ulaya kwa ajili ya wakimbizi wa Syria walioko Uturuki.

Taarifa iliyotolewa leo na WFP imesema kwamba msaada huo utawasaidia waSyria zaidi ya 700,000, wakiwemo nusu milioni wanaoishi nje ya kambi za wakimbizi, wakikumbwa na hali ngumu ya maisha.

WFP imeeleza kwamba idadi hiyo ni mara tatu idadi ya watu wanaosaidiwa sasa hivi kabla ya kupata msaada huo, ambao utawasaidia sana kukabiliana na ongezeko kubwa la idadi ya wakimbizi kutoka Syria nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa WFP, idadi ya wakimbizi wa Syria waliotafuta hifadhi nchini Uturuki ni milioni 2.6.