Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti wabaini uhusiano kati ya Zika na ugonjwa wa misuli kukosa nguvu

Utafiti wabaini uhusiano kati ya Zika na ugonjwa wa misuli kukosa nguvu

Utafiti wa hivi karibuni zaidi uliofanywa katika visiwa vya French Polynesia umebaini uhusiano kati ya kirusi cha Zika kusababisha ugonjwa wa misuli kukosa nguvu, Guillain–Barré .

Mkurugenzi Msaidizi wa WHO anayehusika na dharura za magonjwa Dkt. Bruce Aylward amebainisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari wakati huu ambapo kirusi cha Zika kimeenea katika nchi 47, Tisa kati ya hizo ikiwemo Brazil na French Polynesia zikitaja uhusiano kati kirusi hicho na ugonjwa wa Guillain–Barré.

Dkt, Aylward amesema utafiti umechapishwa katika jarida la Lancet ambapo baadhi ya wagonjwa wa Guillain–Barré wakati wa mlipuko wa Zika huko French Polynesia walichunguzwa sambamba na wale ambao hawakuwa na ugonjwa huo na walichogundua...

(Sauti ya Dkt. Aylward)

“Uwezekano wa kupata kirusi cha Zika kwa mtu mwenye Guillain–Barré ulikuwa mara 35 zaidi kuliko asiye nacho, na huu ni ushahidi wa ngazi ya juu kabisa hadi sasa unaoonyesha uhusiano wa kusababisha ugonjwa.”