Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini DRC, wanawake ni wengi kuliko wanaume, kwanini hawapewi nafasi sawa?

Nchini DRC, wanawake ni wengi kuliko wanaume, kwanini hawapewi nafasi sawa?

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, usawa wa kijinsia bado ni changamoto. Wanawake wanashikilia asilimia 9 tu ya viti vya bunge na chini ya asilimia 5 ya viti vya senate kwa mujibu wa Umoja wa Wabunge Dunaini, IPU. Kadhalika, vita viliyoikumba mashariki mwa nchi hiyo tangu mwaka 1996 vimesababisha mateso mengi hasa kwa wanawake ambao wamekuwa wahanga wa ubakaji na ukatili wa kingono uliotumiwa kama silaha ya vita.

Ni hayo anayaelezea Pascaline Zamuda, mwanaharakati wa haki ambaye mwaka 2010 amepewa tuzo na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kwa kazi zake za uandishi wa habari kuhusu ukatili wa kingono, Mwenyewe amekuwa mkimbizi wa ndani wakati wa vita, lakini sasa anafanyakazi kwenye ofisi ya waziri mkuu wa DRC.

Kwenye mahijiano hayo anaanza kumwelezea Priscilla LEcomte wa idhaa hii changamoto zinazoikumba wanawake nchini DRC