Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ziarani Hispania akitokea Uswisi, baadaye kuelekea Burkina Faso

Ban ziarani Hispania akitokea Uswisi, baadaye kuelekea Burkina Faso

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasili Madrid, Hispania akitokea Geneva, Uswisi.

Habari zinasema akiwa Hispania atakuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje Jose-Manuel Garcia-Margallo ambapo watajadili masuala kadhaa ikiwemo Libya, Syria na Sahara Magharibi kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Mapema akiwa Geneva, Ban alizindua chumba cha Urusi kilichokarabati nchi hiyo katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva, ambapo ameshukuru Urusi siyo tu kwa kusaidia ukarabati huo bali katika ushiriki wake wa masuala ya kisiaisa ikiwepo ushawishi kwenye mpango wa nyuklia wa Iran.

Halikadhalika amegusia ushiriki wa Urusi kwenye kusaka suluhu ya mzozo wa Syria kwa ushirikiano na mataita mengine akisema ni ishara ya nafasi ya mashauriano katika kuleta amani.

Katibu Mkuu alikuwa na mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov ambapo walijadili suala la DPRK na Ukraine akisisitiza umuhimu wa kusongesha mbele utekelezaji wa mkataba wa Minsk.