MINUSCA yafundisha polisi ya CAR kulinda raia dhidi ya ukatili wa kingono

MINUSCA yafundisha polisi ya CAR kulinda raia dhidi ya ukatili wa kingono

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo umehitimisha mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia kwa ajili ya vikosi vya usalama na polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya MINUSCA, polisi 45 wamefundishwa na MINUSCA kuhusu jinsi ya kulinda raia na kukuza maadili miongoni mwa vikosi vya usalama vya serikali. Baada ya hayo waliofundishwa watakuwa na jukumu la kufudisha wenzao.

Mkuu wa polisi ya MINUSCA Luis Carrilho amesisitiza umuhimu wa mafunzo hayo.

(Sauti ya Kamishna Carrilho)

“ Polisi wa MINUSCA wataendela kushirikiana na polisi wa CAR na vikosi vya usalama vya kitaifa ili kuimarisha na kuongeza uwezo wake na kuweza kuhudumia kwa pamoja raia wa CAR kwa njia bora »