Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi yaongezeka mara kumi ikilinganishwa na mwaka 2015

Idadi ya wakimbizi yaongezeka mara kumi ikilinganishwa na mwaka 2015

Idadi ya wakimbizi na wahamiaji wanaowasili Ugiriki na Italia tayari imezidi 120,000 kwa mwaka 2016, theluthi moja wakiwa ni watoto.

Idadi hiyo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka 2015, ambapo kufikia mwisho wa Februari mwaka jana idadi ya waliokuwa wamewasili Ulaya ilikuwa ni 11,800 tu.

Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM ambalo limesema watu 418 wamefariki dunia wakijaribu kuvuka bahari ya Mediteranea mwaka huu.

Itayi Viriri ni msemaji wa IOM

" Tatizo kubwa tunaloshuhudia hasa Italia ni ongezeko la wahamijai wanaokufa kwa kukosa pumzi. Yaani boti wanazosafiria zimejaa mno na watu zaidi wanabanwa kwenye hizo boti, hasa Libya ambako hakuna mamlaka za kuwazuia wahalifu kuingiza watu kwenye boti zilizojaa mno. "