Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leila Zerrougui ajadili ulinzi wa watoto Afghanistan

Leila Zerrougui ajadili ulinzi wa watoto Afghanistan

Mapema wiki hii Bi Leila Zerrougui, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye maeneo ya vita amehitimisha ziara yake nchini Afghanistan. Grace Kaneiya na taarifa Zaidi

(TAARIFA YA GRACE)

Akiwa nchini humo Bi Zerreougui  amejadili na viongozi utekelezaji wa mipango ya serikali kwa ajili ya kuwalinda watoto walioathirika na vita.

Kwa mujibu wa Bi Zerreougui serikali ya Afghanistan inapiga hatua na mipango inaendelea kwa msaada wa Umoja wa Mataifa lakini bado juhudi zaidi zinahitajika kuhakikisha watoto wanalindwa.

(SAUTI YA ZERROUGUI)

"Kuhusu Afghanistan, kuna mzozo unaoendelea kwa muda mrefu,idadi kubwa ya watoto wameuwawa. MMoja kati  ya watu wanne waliouwawa mwaka 2015 ni mtoto, kadhalika kuna ukatili wa aina nyingine unaoathiri watoto nchini Afghanistan ambao ni mashambulizi dhidi ya shule na hospitali. Kwa jumla watu wote wameathirika kwa kiasi kikubwa na mzozo lakini wasichana ndio wahanga wakubwa."