Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO, Tanzania waandaa miongozo ya kubaini virusi vya Zika

WHO, Tanzania waandaa miongozo ya kubaini virusi vya Zika

Shirika la afya ulimwenguni WHO na wizara ya afya ya Tanzania wanaandaa miongozo ya kusaidia kubaini iwapo kuna visa vya virusi vya zika nchini humo kama njia ya kudhibiti ugonjwa huo unaozidi kuenea kwa kasi na tayari umethibitishwa  nchini Cabo Verde.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini Tanzania Dkt. Janeth Mghamba amefafanua maeneo ambayo miongozo hiyo itajikita.

(SAUTI DK JANETH)

Dk Janeth pia anaeleza lini hasa majaribio ya kubaini  maamubukizi ya virusi vya Zika yatafanyika.

(SAUTI DK JANETH)