Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon ampongeza Rais Kenyatta kwa juhudi zake Somalia

Ban Ki-moon ampongeza Rais Kenyatta kwa juhudi zake Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia hali ya usalama nchini Somalia na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, akishukuru mchango wa Kenya katika ujenzi wa amani nchini Somalia, na kusisitiza umuhimu wa kuwa na mkakati thabiti wa kupambana na mizizi ya itikadi kali na katili.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo kando ya mkutano wa 26 wa Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia.

Viongozi hawa wawili wamejadiliana kuhusu mafanikio yaliyopatikana nchini Somalia, na kusisitiza umuhimu wa kuongeza bidii ili kuimarisha ufanisi wa vikosi vya usalama vya kitaifa na taasisi za serikali ili serikali ya Somalia iwe na uwezo wa kutawala kwenye maeneo yote ya nchi.

Aidha wamezungumzia umuhimu wa kuongeza msaada kwa Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini humo, AMISOM.