Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha uteuzi wa mawaziri wa mkataba wa kitaifa Libya

Ban akaribisha uteuzi wa mawaziri wa mkataba wa kitaifa Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo la baraza la Urais la uteuzi wa mawaziri kwa ajili ya serikali ya mkataba wa kitaifa ya Libya.

Amesema hii ni hatua kubwa katika kuelekea utekelezaji wa makubaliano ya kisiasa na suluhu ya mgogoro wa nchi hiyo. Katibu Mkuu amesema anatarajia kupitishwa kwa serikali mpya ili ianze kushughulikia changamoto zinazoikabili nchi hiyo.

Amelipongeza baraza la Urais  na viongozi wote wa Libyaambao wameonyesha nia ya kujidhatiti kwa kuweka maslahi ya taifa kwanza na kujihusisha  na mazungumzo ili kutatua tofauti zao.

Amewataka Walibya wote kuunga mkono utekelezaji wa makuabaliano ya kisiasa nchini humo ili Libya iendelee na kipindi cha mpito cha kidemokrasia.