Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Slovenia na UNICEF washirikiana kusaidia watoto wahamiaji na wakimbizi:

Slovenia na UNICEF washirikiana kusaidia watoto wahamiaji na wakimbizi:

Ikiwa wahamiaji na wakimbizi 3000 wanapitia Slovenia kila siku , shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na serikali ya Slovenia leo wametangaza ushirika wenye lengo la kuboresha huduma na ulinzi kwa watoto wanaokimbia.

Wakati idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji wanakaa kwa muda mfupi Slovenia kabla ya kuendelea na safari yao, bado mahitaji yao ya kibinadami nui makubwa hususan kwa wale wasiojiweza wakiwemo watoto amesema Boštjan Šefic, Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu Huduma kwa Wakimbizi wa Slovenia.

Ameongeza kuwa ndio maana wanashirikiana na UNICEF ili kuimarisha msaada na huduma kwa watoto na famialia wakati wakiendelea na safari zao kupitia Slovenia na zaidi.

Licha ya juhudi za serikali kutoa malazi na huduma muhimu kwa watu wanaoendelea na safari mfumo wa msaada umeshikika kutokana na ukubwa wa tatizo, na UNICEF ina lengo la kuimarisha na kuongeza ulinzi kwa watoto nchini Slovenia, lakini pia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wanaotoa huduma wakati huu wa majira ya baridi.