Skip to main content

Hadi sasa hakuna uhusiano kati ya Zika na watoto wenye vichwa vidogo- WHO

Hadi sasa hakuna uhusiano kati ya Zika na watoto wenye vichwa vidogo- WHO

Shirika la afya duniani, WHO linafuatilia kwa karibu taarifa za uwepo wa kirusi aina ya Zika katika mataifa 18 duniani, kirusi ambacho kinadaiwa kuwa na uhusiano na watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo.

WHO imesema kirusi hicho kinachoenezwa na mbu aina ya Aedes, kimeripotiwa katika mataifa ya Amerika, Afrika na Pasifiki Magharibi na ndicho kinachosababisha ugonjwa wa Dengeu, Chikungunya na homa ya manjano.

Afisa kutoka WHO Christian Lindmeier amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa visa vya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo vinaongezeka Brazil ambapo kati ya mwaka 2010 na 2014 kwa wastani kila mwaka watoto 163 huzaliwa na kasoro hiyo.

Hata hivyo amesema..

Ijapokuwa kuna ongezeko la visa hivyo, bado haijathibitishwa kuwepo kwa uhusiano kati ya kirusi cha Zika na watoto kuzaliwa na vichwa vidogo. WHO inaainisha na kusaidia maeneo ya utafiti zaidi na kutoa wito kwa nchi wanachama kukusanya na kubadilishana taarifa na wizara za afya baina  yao juu ya mlipuko wa kirusi hicho. “

Kwa mujibu wa WHO hadi sasa hakuna chanjo dhidi ya kirusi hicho chenye asili ya msimu wa Zika nchini Uganda, na WHO inatoa wito kwa serikali kuhakikisha watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo wanafanyiwa tathmini ya kutosha na ufuatiliaji kwa kuwa hakuna tiba mahsusi.