Skip to main content

UNMISS yakutanisha upinzani na jamii ya wakimbizi wa ndani

UNMISS yakutanisha upinzani na jamii ya wakimbizi wa ndani

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, Ellen Margrethe Løj, amekariri dhamira ya ujumbe huo ya kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano ya amani kuhusu kuutanzua mzozo nchini humo.

Bi Margrethe Løj amesema hayo akifungua mkutano wa wajumbe wa SPLM Upinzani na wawakilishi wa watu waliolazimika kuhama makwao katika kituo cha ulinzi wa raia mjini Juba.

Katika mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Juba, Bi Margrethe Løj amesema dhamira kuu ya ujumbe huo ni kuwalinda raia wanaohitaji ulinzi katika vituo vya ulinzi wa raia, na kuwahakikishia usalama waliokimbilia vituo hivyo.

“Kwangu mimi, waliotafuta hifadhi katika kituo chetu cha ulinzi wa raia, ni watu wanaohitaji ulinzi, bila kujali kabila au wanapoegemea kisiasa. Naweka umuhimu mkubwa katika kuhakikisha kuwa hakuna shughuli za kisiasa katika vituo vya ulinzi wa raia Juba au kwingineko kule,