Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliojitokeza kushiriki uchaguzi wa CAR ni 75%- MINUSCA

Waliojitokeza kushiriki uchaguzi wa CAR ni 75%- MINUSCA

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA umeripoti kuwa Mamlaka ya Kitaifa ya Uchaguzi ANE imetangaza baadhi ya matokeo ya uchaguzi siku ya Jumapili hii kulingana na kura zilizopigwa kwenye majimbo nane na asilimia 15 ya kura zilizopigwa nje ya nchi.

Hii ni kwa mujibu wa Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric ambaye amewaambia leo waandishi wa habari mjini New York Marekani kwamba matokeo kamili yanatarajiwa kutolewa mwisho wa wiki hii na kuthibitishwa na Mahakama ya Kikatiba tarehe 15 Januari.

Aidha amesema kwamba MINUSCA imeripoti kuwa asilimia 95 ya vituo vya kupigia kura vilikuwa vimefunguliwa siku ya uchaguzi huku takriban asilimia 75 ya watu wakiwa wamejitokeza kupiga kura.

Hata hivyo ameongeza kwamba jumatatu hii baadhi ya wagombea urais wamezungumza na waandishi wa habari ili kulaani makosa kadhaa ya kiufundi katika mchakato wa uchaguzi.