UNICEF/UNRWA kusaidia watoto wa Palestina msimu wa baridi

23 Disemba 2015

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limetangaza kusambaza misaada kwa ajili ya msimu wa baridi kwa watoto wakimbizi wa Palestina wanaoishi nchini Lebanon kwa ushirikiano na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina UNRWA.

Kwenye taarifa yake UNRWA imeeleza kwamba misaada hiyo imetolewa kupitia kadi za ATM ikiwa ni sawa na dola 40 za kimarekani kwa kila mtoto ili kuwezesha wazazi wa watoto hao kuwanunulia nguo za kujisitiri baridi kali.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Lebanon Tanya Chapuisat ameongeza kwamba wakimbizi wa Palestina wanaoishi Lebanon wanakumbwa na baridi kali zaidi kwani baadhi yao huishi kwenye maeneo ya milima.

Kwa ujumla UNICEF imechangia dola milioni 7 tangu mwaka 2013 kwa watoto wakimbizi wa Palestina kwa ajili ya huduma za elimu, afya, maji na usafi pamoja na ulinzi dhidi ya ukatili.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter