Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umefadhaishwa na msamaha na uteuzi wa mbakaji kuwa balozi Zambia

UM umefadhaishwa na msamaha na uteuzi wa mbakaji kuwa balozi Zambia

Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Zambia kudhihirisha imejidhatiti katika jitihada zake za kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana na kukomesha ukatili uliofanywa na muimbaji wa Zambia Clifford Dimba, ambaye alikuwa na hatia ya kumbaka msichana wa miaka 14 kwa 2014 mwaka 2014 na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 18 jela.

Bwana Dimba amepewa msamaha na Rais Lungu baada ya kutumikia mwaka mmoja tuu wa hukumu yake na kisha kuteuliwa kuwa balozi katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Wataalamu hao wanaitaka serikali ya Zambia kuufuta uteuzi wa Bwana Dimba na kuhakikisha kwamba hakuna msamaha mwingine tena kwa makosa kama hayo ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

Kwa mujibu wa Dubravka Šimonovic’ mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake, sababu na athari zake kuachiliwa kwa Dimba na uteuzi wake kama balozi dhidi ya ukatili sio utatonesha kidonda kwa muathirika upya bali pia utawakatisha tamaa waathirika wengine kutoa taarifa za makosa kama hayo.

Naye mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uuzaji, Ukahaba na Ngono kwa Watoto, Maud de Boer-Buquicchio,amesema msamaha huo kwa bwana Dimba na ukwepaji wa sheria unaongeza madhila zaidi badala ya kuyapunguza.