Ban asikitishwa na kuuwawa kwa wakimbizi wa Sudan

Ban asikitishwa na kuuwawa kwa wakimbizi wa Sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mauaji ya wakimbizi watano wa Sudan yaliyotekelezwa na vikosi vya usalama vya Misri mpakani mwa nchi hiyo na Israel.

Wakimbizi wengine sita wamejeruhuiwa katika  tukio hilo.

Msemaji wa Ban Stéphane Dujarric  amewaambia waandishi wa habari mjni New York kuwa tukio hilo linafuatia mauaji ya wakimbizi wengine 15 ambapo  wengine wanane walijeruhiwa juma moja lilopita.

(SAUTI DUJJARIC)

‘Katibu Mkuu ameitaka mamlaka nchini Misri kuanzisha uchunguzi kamili lili kupata taarifa kamili kuhusu tukio hilo ili kuhakikisha uwajibikaji na kuzuia  kujirudia matukio hayo.’’