Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi yajadiliwa kwenye mkutano kuhusu uhamiaji, Baraza la Usalama

Burundi yajadiliwa kwenye mkutano kuhusu uhamiaji, Baraza la Usalama

Viongozi wanaoshiriki mkutano wa viongozi wa Ulaya na Afrika kuhusu uhamiaji mjini Valetta, Malta wameeleza kutiwa wasiwasi na migawanyo inayozidi kupanuka nchini Burundi, ikitishia kuhatarisha maisha ya watu wengi zaidi na uwezekano wa mzozo mkubwa kikanda. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte

(Taarifa ya Priscilla)

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU, Nkosazana Dlamini-Zuma na Mwakilishi wa EU wa ngazi ya juu, Federica Mogherini, viongozi hao wameahidi kushirikiana na kutumia njia zote ili kuzuia hali nchini Burundi kuzorota zaidi.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa viongozi hao wamekubaliana kuhusu haja ya dharura ya kuitisha mkutano wa serikali ya Burundi na upinzani mjini Addis Ababa, Ethiopia au Kampala, Uganda, chini ya uwenyekiti wa Rais Museveni ili kupata suluhu la kisiasa.

Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo Alhamis kujadili hali nchini Burundi.