Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Intaneti nyenzo muafaka kwa maendeleo endelevu : Lenni Montiel

Intaneti nyenzo muafaka kwa maendeleo endelevu : Lenni Montiel

Mkutano wa siku tatu wa jukwaa la usimamizi wa intaneti (IGF) ,  unaohusisha maafisa wa ngazi za juu wa serikali, viongozi wa asasi za kiraia na wataalamu wa sera za intaneti umeanza leo nchini Brazil, ukijadili jukumu muhimu la mtandao huo  katika kufanikisha utekelezaji wa ajenda 2030 ya malengo endelevu.

Akiongea mjini New York katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa muda mfupi kabla ya kuelekea Brazil, msaidizi wa Katibu Mkuu wa UM katika idara ya uchumi na masuala ya kijamii Lenni Montiel amesema mtandao wa intanet ni chombo muhimu katika kusukuma maendeleo kimataifa.

(SAUTI LENNI MONTIEL)

‘‘Jukwaa la intaneti ni fursa muhimu inayotumiwa na jumuiya ya kimataifa tangu mwaka 2006 katika kukutana na kujadili mambo yahusuyo namna nchi wanachama wa UM, asasi za kiraia, na sekta binafsi zinavyoweza kuingiliana na kukubaliana namana ya kufanya kazi katika intaneti.’’

IGF inakuja wakati ambapo malengo ya maendeleo endelvu yamepitishwa hivi karibuni ambayo yanasisitiza umuhimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano na intaneti katika shughuli za maendeleo.