Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya wanahabari Syria na Bangladesh

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya wanahabari Syria na Bangladesh

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokova, amelaani mauaji ya wanahabari wawili wa Syria ambao walikutwa maiti mnamo 30 mwezi Oktoba, katika mji wa Sanlıurfa Kusini Mashariki ya Uturuki. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Akilaani mauaji ya Ibrahim Abdel Qader na Fares Hammadi, Bi. Bokova amezitaka mamlaka zote kufanya kila juhudi kuhakikisha kwamba wauaji hao wamewajibishwa kisheria.

Ameongezea kuwa ni lazima wafanye kila wawezalo kulinda wanahabari dhidi ya vikundi vyenye misimamo mikali vilivyo tayari kuua na kukandamiza haki ya watu ya kupata habari.

Wakati huohuo, Bokova ametaka uchunguzi wa haraka ufanywe kuhusu mauaji ya Mchapishaji wa Bangladeshi, Faisal Arefin Dipan mnamo 31 Oktoba baada ya kuuawa kwa mwandishi wake, Avijit Roy mapema mwaka huu.