Skip to main content

Wasiwasi kuhusu mapigano kati ya polisi na waandamanaji Congo

Wasiwasi kuhusu mapigano kati ya polisi na waandamanaji Congo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepokea na wasiwasi ripoti za mapigano kati ya waandamaji na polisi huko Brazzaville mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, kabla ya kura ya maoni iliyofanyika jumapili hii, tarehe 25 nchini humo.

Hii ni kwa mujibu wa msemaji wake Stephane Dujarric alipozungumza leo na waandishi wa habari mjini New York, akisema kwamba Bwana Ban ameelezea pia wasiwasi wake kuhusu kufungwa kwa baadhi ya viongozi wa upinzani.

Ameongeza kwamba serikali inapaswa kuwajibika ili kuhakikishia haki za raia za kujieleza huru na kuandamana kwa amani, akizisihi mamlaka za serikali kujizuia na kutumia ghasia dhidi ya maandamano.

Bwana Dujarric ameeleza pia kwamba Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kwa Afrika ya Kati, Abdoulaye Bathily, alikwenda Brazzaville siku chache kabla ya kura hiyo ili ahamasishe mazungumzo baina ya wadau wote.

Ametoa wito pia pande zote zishiriki mazungumzo kuhusu mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.