Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Magenge ya usafirishaji haramu wa watu yadhibitiwe:Ban

Magenge ya usafirishaji haramu wa watu yadhibitiwe:Ban

Vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu vimeendelea kuwafadisha magenge machache ya watu huku wanawake na watoto wakiendelea kuwa wahanga wakubwa wa matukio hayo.

Inakadiriwa kwamba kwa mwaka magenge hayo yanayoendesha biashara ya kusafirisha watu huvuna kiasi cha dola bilioni 32. Watu wanaosafirishwa kila mwaka duniani kote wanasadikika kufikia kati ya 600 mpaka 800 .

Tayari jumuiya za kimataifa zimeanza kusaka mbinu za haraka kudhibiti hali hiyo. Hivi sasa huko Luxor, Misri, viongozi wa mataifa mbalimbali wameanza kukutana kujadilia mbinu za kukabili wimbi hilo la usafirishaji haramu wa binadamu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amempongeza mke wa wa rais Misri Suzanne Mubarak kwa kuandaa kongamano hilo. Ban ametaka makundi yanayoendesha biashara hiyo yapewa mbinyo zaidi.