Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uamuzi wa ZEC hauathiri kutangazwa matokeo Tanzania:NEC

Uamuzi wa ZEC hauathiri kutangazwa matokeo Tanzania:NEC

Kufuatia Tume ya uchaguzi Zanzibar, ZEC kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi, Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Tanzania, NEC imesema hatua  hiyo haina athari yoyote katika uchaguzi uliofanyika Tanzania Bara.

Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguza Tanzania, Jaji mstaafu Damian Lubuva ametoa tamko  hilo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam muda mfupi baada ya Tume ya uchaguzi Zanzibar kutangaza uamuzi wake.

(Sauti ya Jaji mstaafu Lubuva)