Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yalaani mashambulizi Afghanistan

Ofisi ya haki za binadamu yalaani mashambulizi Afghanistan

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zeid Ra’ad al Hussein amelaani vikali mashambulizi dhidi ya Tume huru ya Haki za Binadamu ya Afghanistan yaliyotokea leo mjini Jalalabad ambapo watu wawili wameuawa na wengine 6 kujeruhiwa.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, Kamishna Zeid amesema tume hiyo ilikuwa inajitahidi kufuatilia hali ya haki za binadamu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 na kupambana na shinikizo kutoka kwa serikali na upinzani.

Ameongeza kuwa mashambulizi hayo ni mashambulizi dhidi ya raia wa Afghanistan akitumai kwamba tume hiyo itaendelea kufanya kazi kwa nguvu na ufanisi mkubwa zaidi.

Kwa upande wake ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani pia mashambulizi haya ukisisitiza kwamba mashambulizi dhidi ya raia ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na sawa na mauaji ya kivita.