Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tetemeko la ardhi laathiri Afghanistan na Pakistan- OCHA

Tetemeko la ardhi laathiri Afghanistan na Pakistan- OCHA

Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA, imesema kwamba hadi sasa ni vigumu kupata ripoti kamili kutoka Afghanistan kwa sababu mawasialiano ya simu yamekatika. Aidha baadhi ya barabara kubwa zimefungwa kwa sababu ya maporomoko ya ardhi.

Kwa mujibu wa OCHA, uharibifu si mkubwa sana nchini Afghanistan, watu wanaoishi kwenye maeneo husika wakiwa ni wachache.

Nchini Pakistan, watu angalau 148 wameuawa na wengine 815 kujeruhiwa.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wale wameanza kukusanya vifaa vya dharura kwa ajili ya kusaidia jitihada za serikali.