Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa

Kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa

Miaka 70 ya Umoja wa Mataifa imeadhimishwa maeneo mbali mbali duniani kwa nchi wanachama kushiriki matukio kadhaa ikiwemo kuangazia rangi ya buluu kwenye majengo na minara mashuhuri kuonyesha mshikamano na chombo hicho kilichoanzishwa miongo saba iliiyopita.

Makao makuu ya Umoja wa Mataifa nayo hayakuwa nyuma kwani usiku wa tarehe 23 Oktoba, ikiwa ni mkesha kuelekea kilele tarehe 24 Oktoba onyesho maalum la muziki lilifanyika kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likileta pamoja waimbaji kwaya kutoka Korea Kusini, Harlem New York, halikadhalika waimbaji mtindo wa pop kutoka Korea Kusini na mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa. Je nini kilifanyika? Assumpta Massoi anakufafanulia kwenye makala hii.