Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyama ya ngombe, nguruwe, mbuzi na soseji husababisha saratani : utafiti

Nyama ya ngombe, nguruwe, mbuzi na soseji husababisha saratani : utafiti

Shirika la Kimataifa la Utafiti kuhusu saratani, IARC,  limetoa ripoti leo ikionyesha kwamba kula nyama nyekundu na nyama zilizosindikwa kunaweza kusababisha saratani.Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo, kula gramu 50 ya nyama zilizosindikwa kila siku huongeza hatari ya saratani ya utumbo kwa asilimia 18.

Daktari Kurt Straif ni mkuu wa idara ya utafiti ya IARC.

(Sauti ya Dkt. Straif)

"Hatari ni ndogo, ni kama hatari ya kuugua saratani ya mapafu kutokana na kukaribia mvutaji sigara, lakini tunapaswa kujua kwamba watu wengi wanakula nyama nyekundu au ya kusindikwa kwa hiyo ni tatizo la afya ya umma. "

Aina zingine za saratani zinazoweza kusababishwa na aina hizo za nyama ni saratani ya kongosho na ya kibofu.

IARC imependekeza watu wapunguze matumizi ya nyama nyekundu na zilizosindikwa.

Nyama nyekundu ni nyama za ngombe, nguruwe, kondoo, na mbuzi. Mifano ya nyama zilizosindikwa ni hotdog, soseji na hemu.