Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visa vipya vya Ebola vyabainika Guinea: WHO

Visa vipya vya Ebola vyabainika Guinea: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO liemesema mapema juma hili visa viwili vya Ebola vimethibitishwa nchini  Guinea baada ya majuma kadhaa ya kutokuwa na visa vipya katika nchi za ukanda wa Afrika Magharibi.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva msemaji wa WHO Margret Harris amesema licha ya habari njema za awali lakini bado wanakabilana na visa vichache kama hivyo lakini akasisitiza kuwa nchi nyingine ine kama Sierra Leone haijathibitika kuwa na kisa kingine tangu mwezi Septemba.

Akifafanua kuhusu matibabu yanayoweza kutowesha kabisa Ebola kwa mgonjwa kwa kuzingatia idadi ya watu walioambukizwa na kunusurika anasema.

(SAUTI)

‘‘Kirusi cha Ebola sio kipya, jambo jipya hapa ni ubora wa kushugulikia manusura katika idadi kubwa iliyojitokeza na idadi kubwa ya wataalamu. Wakati wa milipuko iliyopita ilitumika njia bora ya kutibu wenye hali mbaya kwanza. ‘’