Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na ICAO wakaribisha ripoti ya mwisho ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya MH17

UM na ICAO wakaribisha ripoti ya mwisho ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya MH17

Shirika la Kimataifa la Usalama wa Anga, ICAO leo limekaribisha ripoti ya uchunguzi ya mwisho kuhusu ajali ya ndege ya Shirika la ndege la Malaysia MH17, ripoti ambayo imetolewa na  Bodi ya Usalama ya Uholanzi.

Ripoti hiyo ya mwisho ya uchunguzi wa ajali hiyo ya mwezi Julai mwaka 2014, inatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti na kutoa mapendekezo ya kiufundi uliofanywa chini ya mahitaji ya kimataifa iliyoanzishwa na kimabatanisho namba 13 cha Mkataba wa Biashara ya Usafiri wa Anga.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, kupitia msemaji wake Stéphane Dujarric amesema tangu mwanzo, Umoja wa Mataifa umeunga mkono kikamilifu uchunguzi huo pamoja na azma ya jumuiya ya Kimataifa ya kutafuta ukweli kuhusu kile kilichotokea.  Dujarric alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, na kusema..

(SAUTI Dujarric)

"Katibu Mkuu angependa kwa mara nyingine kutumia fursa hii ya kutolewa kwa ripoti  kuwapa pole waathiriwa wasio na hatia wa ajali ya ndege ya MH17 , watu  wote ambao walipoteza maisha yao siku hiyo. Katibu Mkuu anaunga mkono kwa dhati uwajibikaji kamili  kuhusu janga hilo, na kusisitiza mtu yeyote atakayepatikana na hatia achukuliwe  hatua za kisheria."