Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahudumu wa afya wa jamii hutumia maarifa yao kuokoa maisha katika majanga- WHO

Wahudumu wa afya wa jamii hutumia maarifa yao kuokoa maisha katika majanga- WHO

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya kupunguza hatari za majanga, Shirika la Afya Duniani WHO, limetoa wito kwa watu duniani watambue umuhimu wa wahudumu wa afya wa jamii katika kampeni yake ya #ThanksHealthHero.

WHO imesema wahudumu wa afya wa jamii wanaelewa hatari za kiafya za jamii zao, tabia zao na mienendo yao, na kwamba kutokana na utamaduni, desturi na maadili yao, wanaweza kuchangia pakubwa katika kukabiliana na hatari za kiafya zitokanazo na hali za dharura na majanga.

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa mwaka huu yanamulika mchango wa maarifa na elimu ya kijadi, na jinsi inavyoongeza uthabiti wa jamii, kauli mbiu ikiwa ni “Maarifa kwa Uhai.”