Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sakata la Ashe, Ban aitisha ukaguzi

Sakata la Ashe, Ban aitisha ukaguzi

Kufuatia mashtaka ya tuhuma za rushwa dhidi ya aliyekuwa  Rais wa mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe, yaliyotangazwa na mamlaka ya Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameomba ofisi za ukaguzi wa ndani za umoja huo kuzindua ukaguzi wa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na mfuko wa malengo endelevu na kampuni ya Kian Ip Group na matumizi ya fedha zilizopokelewa kutoka katika taasisi hizi.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, msemaji wa Katibu Mkuu Stephan Dujarric amesema Ban amesikitishwa na ukubwa wa tuhuma ambao unagusa maadili ya kazi ya Umoja wa Mataifa na nchi wanachama.

Stephan amesisitiza wito wa Katibu Mkuu

(SAUTI BAN)

‘‘Katibu Mkuu amekariri kwamba hakutakuwa na uvumilivu kwa rushwa yoyote katika Umoja wa Mataifa au kwa jina la Umoja wa Mataifa. Amejidhatiti kuhakikisha fedha zinazopokelewa kutoka katika taasisi kama hizo zilitumiwa vyema kulingana na sheria na kanuni za Umoja wa Mataifa.’’