Skip to main content

Tupo tayari kushirikiana na dunia katika amani na maendeleo: China

Tupo tayari kushirikiana na dunia katika amani na maendeleo: China

China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika ujenzi wa amani na maendeleo amesema rais wa China Xi Jinping wakati akilihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika mkutano  wake wa 70 unaondelea mjini New York.

Kiongozi huyo amesema kuwa katika kusongesha mbele maendeleo nchi yake iko tayari hushirikiana na nchi nyingine katika masuala ya ujuzi na fursa ili kutimiza malengo ya pamoja ya maendeleo enedelevu SDGs.

(SAUTI JINPING)

‘Tutaendelea kutekeleza sheria za kiamataiaf na mifumo chini ya kanuni za mkataba wa Umoja wa Mataifa. China itaendlea kushirikiana na nchi zinazoendelea kwani tunaunga mkono uwakilishi na sauti za nchi hizi hususani bara la Afrika katika mfumo wa utawala wa kiamataifa.’’

Katika hotuba yake Rais wa China Xi Jinping amesisitiza umhimu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kama seheemu ya kupata maendeleo endelevu.