Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzigo wa kiuchumi kwa ajili ya tabianchi ni mzito kwa bara la Afrika:Prof. Kowero

Mzigo wa kiuchumi kwa ajili ya tabianchi ni mzito kwa bara la Afrika:Prof. Kowero

Athari za kiuchumi kutokana na mabadiliko ya tabianchi kwa bara la Afrika ni nyingi na iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa haraka iwezekanavyo, huenda rasilimali ya misitu ikapotea.

Hiyo ni kauli ya Profesa Godwin Kowero Katibu Mkuu wa African Forest Forum aliyotoa kandoni mwa mkutano wa 14 kuhusu misitu unaoendelea mjini Durban, Afrika Kusini.

Mkutano huo wenye kauli mbiu: "Watu na misitu, kuwekeza katika misitu endelevu" umewaleta watu mbali mbali na serikali kwa ajili ya kuangalia mustakhabali wa misitu endelevu.

Profesa Kowero amesema kutoweka kwa rasilimali hizo kutaathiri maisha ya jamii, kadhalika uwezo wa kiuchumi wa mataifa ya Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hivyo akasema….

“Kuna jamii ambazo zimeweka mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, lakini changamoto hii haiwezi kuachwa kwa jamii, ama hatua za kisayansi zinahitajika kutoka kwa serikali na kwa jamii ya kimataifa kwa sababu iwapo Afrika ina uhakika wa chakula hivyo basi dunia nzima itakuwa na uhakika wa chakula”