Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atiwa wasiwasi ni hali kati ya India na Pakistan

Ban atiwa wasiwasi ni hali kati ya India na Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ameelezwa kutiwa wasiwasi na kuongezeka kwa machafuko hivi karibuni kwenye mpaka wa India na Pakistan, ambayo yalisababisha vifo kwa pande zote, vikiwemo vya raia.

Ban ametuma rambirambi zake kwa familia za wahanga wa machafuko hayo.

Taarifa kutoka ofisi ya msemaji wake imesema kuwa Katibu Mkuu ametoa wito kwa India na Pakistan kudhibiti hisia kali, na kuchukua hatua mathubuti za kuhakikisha kuwa raia wanalindwa.

Aidha, Bwana Ban ametoa wito kwa nchi hizo mbili kushughulikia tofauti zao kupitia kwa mazungumzo, na kukaribisha mkutano wa washauri wa usalama wa kitaifa uliopangwa kufanyika Agosti 23 na 24.