Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maadhimisho ya miaka 70 kupitia utamaduni

Maadhimisho ya miaka 70 kupitia utamaduni

Katika dunia ya leo, uwezo wa utamaduni kubadilisha jamii ni dhahiri. Njia mbali mbali zinazowakilisha utamaduni ikiwemo, majengo ya ukumbusho, usanii na mila na desturi zina umuhimu katika maisha ya kila siku kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO.

Utamaduni unatambulika kama chanzo cha kuchagiza uwiano katika jamii na ni muhimu katika kubadilisha maisha ikiwemo kiuchumi. Ni kwa dhamira hiyo ambapo katika harakazi za kuadhimisha miaka sabini ya Umoja wa Mataifa kumefanyika hafla maalum ambayo iliwaleta watu wa bara Asia na Afrika pamoja kupitia utamaduni. Joshua Mmali anasimulia