Baraza la Usalama lajadili ripoti ya uchunguzi kuhusu ajali ya ndege ya Malaysia nchini Ukraine

20 Julai 2015

Baraza la Usalama leo limekuwa na mjadala wa faragha kuhusu ajali ya ndege ya Malaysia iliyotunguliwa nchini Ukraine mwaka mmoja uliopita, likijadili kuhusu ripoti ya kamati ya uchunguzi na kuzungumzia pendekezo lake la kuunda mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu huo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Rais wa Baraza la Usalama na Mwakilishi wa Kudumu wa New Zealand kwenye Umoja wa Mataifa Gerard van Bohemen amesema wanachama wengi wameunga mkono pendekezo hilo, isipokuwa Urusi, akieleza matumaini yake ya kufikia makubaliano kuhusu swala hilo.

Ndege ya Malaysia MH17 ilitunguliwa tarehe 17 Julai mwaka 2014 kwenye tukio lililosababisha vifo vya watu 298.

Wakati wa kuadhimisha mwaka mmoja tangu tukio hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni lazima ukweli ujulikane na waliotekeleza uhalifu huo wawajibishwe.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter