Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon alaani shambulizi la kigaidi Uturuki

Ban Ki-moon alaani shambulizi la kigaidi Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililotokea leo mjini Suruc, nchini Uturuki, na ambalo limesababisha vifo vya watu wapatao 28 na mamia ya wengine kujeruhiwa.

Katika taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, Bwana Ban amenukuliwa akisema hakuna sababu yoyote inayoweza kuruhusu kulenga raia wa kawaida.

Katibu Mkuu amesema anatumaini kwamba watekelezaji wa uhalifu huo watabainiwa haraka na kupelekwa mbele ya sheria. Aidha ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga, pamoja na serikali na raia wa Uturuki, akiwatakia nafuu waliojeruhiwa.