Skip to main content

Mtalaam wa UM aiomba Eritrea kuheshimu haki za binadamu

Mtalaam wa UM aiomba Eritrea kuheshimu haki za binadamu

Leo Baraza la Haki za Binadamu limeendelea kujadili hali ya haki za bindamau nchini Eritrea, Mratibu Maalum kuhusu haki za binadamu nchini humo, Bi Sheila Keetharuth akiwasilisha ripoti yake inayomulika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu Eritrea, baada ya mwenyekiti wa kamisheni ya uchunguzi kuwasilisha ripoti yake hapo jana. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Bi Keetharuth leo ameeleza kwamba mamia ya familia zimefukuzwa kwao kwa madai ya kwamba hawakuwa na ruhusa ya kujenga, huku nyumba zao zikibomolewa. Aidha amemulika hali ya vijana ambao wanaikimbia nchi yao kwa sababu wanaogopa kutumikishwa jeshini kwa muda usiojulikana.

Akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuisaidia Eritrea kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba na kufuatilia vijana wadogo wanaojaribu kuihama nchi bila kusindikizwa na mtu yeyote, Mratibu huyo maalum akatoa wito pia kwa serikali ya Eritrea.

“ Tunapaswa kuona hatua, kuliko ahadi zisizo kuwa kamili, kwamba serikali ya Eritrea inataka kutekeleza wajibu wake kuhusu haki ya kimataifa ya binadamu”

Kwa upande wake serikali ya Eritrea imekanusha kinchosemwa na ripoti hiyo, ikisisitiza kwamba raia wake wanashiriki ipasavyo kwenye maswala ya kisiasa.