Skip to main content

Baraza kuu lapitisha June 19 siku ya kupinga unyanyasaji wa kingono kwa wanawake vitani

Baraza kuu lapitisha June 19 siku ya kupinga unyanyasaji wa kingono kwa wanawake vitani

Baraza kuu leo limepitisha azimio kwamba Juni 19 kila mwaka itakuwa siku ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kingono katika maeneo yenye migogoro ili kusongesha mbele kampeni dhidi ya vitendo hivyo. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(TAARIFA YA JOSEPH MSAMI)

Azimio hilo ni juhudi za mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukatili wa kingono kwenye maeneo ya kivita Hawa Bangura pamoja na nchi kadhaa ikiwamo Argentina na asasi za kiraia.

Akipitisha azimio la kuwepo kwa siku hiyo Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa amesema kile ambacho ni muhimu katika ukomeshwaji wa ukatili wa kingono katika maeneo yenye vita.

(SAUTI KUTESA)

‘‘Katika nchi yangu Uganda kulikuwa na zama ambapo vitendo vibaya sana vilitendwa ikiwamo utekwaji wa watoto, uuwaji wa wanaume na ubakaji kwa wanawake. Sio tu kwamba tulipinga lakini pia raia waliishinikiza serikali kuwachukulia hatua watakelezaji. Lazima tuhakikishe kuwa watekelezaaji wa uhalifu huu wanawajibishwa na waathiriwa wanapata haki yao’’.

Hata hivyo amesisistiza ujumuishwaji kikamilifu na kwa usawa kwa  wanawake katika ujenzi wa amani hususani katika kutafuta suluhu la migogoro pamoja na ukomeshwaji wa ukatili wa kingono.