Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kibiandamu Yazidi kuzorota Sudan Kusini: OCHA

Hali ya kibiandamu Yazidi kuzorota Sudan Kusini: OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kibinadamu OCHA imesema kuwa hali ya kibinadamu nchini Sudan Kusini inaendelea kuzorota, watu wanaendelea kuwa katika mazingira hatarishi na kiwango cha upungufu wa chakula kinaendelea kukua.

Taarifa ya OCHA insema kuwa uwezo wa jamii ya watu nchini humo kuishi huku wakitegemea misaada baada ya machafuko umefikiwa mwisho ilihali ukosefu wa chakula umekuwa kwa kasi kubwa ambapo watu milioni 4.6 watakumbwa na janga la kibinadamu kuhitaji misaada ya dharura ifikapo mwezi Julai.

Kwa mujibu wa OCHA hiki ni kiwango kikubwa zaidi tangu kuanza kwa machafuko nchini Sudani Kusini.

Taarifa hiyo imesema pia kuwa mkutano wa ngazi ya juu unaofanyika mjini Geneva juma lijalo Juni 16 utaleta pamoja wadau wa misaada ya kibinadamu na maendeleo na wahisani muhimu ili kutoa uelewa ziadi kuhusu hali ilivyo Sudan Kusini na eneo zima .

 Mkutano huo pia unatarajiwa kushugulikia ukosefu wa fedha katika operesheni za kibinadamu nchini humo.