Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaungana na klabu ya Juventus kuendeleza miradi ya uiano wa kijamii CAR

UNESCO yaungana na klabu ya Juventus kuendeleza miradi ya uiano wa kijamii CAR

Ujumbe wa pamoja wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na klabu ya soka ya Juventus kutoka Italia, unazuru Jamhuri ya Afrika ya Kati wiki hii ili kujionea maendeleo ya miradi waliyoanzisha kwa pamoja ili kuwasaidia watoto walioathirika na mzozo nchini humo kujiunga tena na jamii.

Ujumbe huo ambao unaongozwa na Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Eric Falt na Rais wa Magwiji wa zamani wa Juventus, David Trézéguet, tayari umejionea kazi iliyomazilika katika miezi ya kwanza ya mradi huo.

Watoto 100 walichaguliwa kunufaika na mradi huo katika awamu ya kwanza, wakipata kwanza mafunzo ya kusoma na kuandika, na kisha kupewa mafunzo ya kitaaluma, yakiwemo kutengeza bidhaa za ngozi, kulehemu, kushona vikapu na uchongaji bidhaa za mbao.

Watoto waliochaguliwa na wale waliokuwa wameshurutishwa kutumika vitani, na ambao waliathiriwa kimwili na kimaadili.