Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka wahudumu wa kibinadamu waachiliwe mara moja Libya

UM wataka wahudumu wa kibinadamu waachiliwe mara moja Libya

Mratibu wa Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Georg Charpentier, ameelezea kusikitishwa na kuendelea kutekwa kwa wahudumu wa kibinadamu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Libya, na kutoa wito waachiliwe mara moja, bila masharti yoyote.

Mratibu huyo ameeleza kuhofia athari za kisa hicho kwa uwezo wa jamii ya kimataifa na mashirika ya wadau wa kufikisha usaidizi unaohitajika mno kwa jamii zilizoathiriwa na mgogoro nchini Libya, wakiwemo wakimbizi wa ndani.

Ametoa wito kwa wale wote wenye wajibu na ushawishi kuingilia kati ili kuhakikisha kuwa wahudumu hao watatu wa kibinadamu wanaachiwa huru, na kuwezesha ufikishaji misaada kwa wahitaji.

Amekumbusha kuwa utekaji nyara na vitisho vya moja kwa moja dhidi ya wahudumu wa kibinadamu wa kiaraia ni uhalifu wa kivita.