Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban na Rais Park wa Korea Kusini wajadili ulinzi wa wakimbizi

Ban na Rais Park wa Korea Kusini wajadili ulinzi wa wakimbizi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, na rais wa Jamhuri ya Korea, Park Geun-hye, wamekutana na kujadili kuhusu mambo mseto, yakiwemo umuhimu wa kupiga hatua kuhusu ajenda ya maendeleo baada ya 2015, mabadiliko ya tabianchi, usaidizi na ufadhili kwa ajili ya maendeleo, ulinzi wa wakimbizi na wahamiaji, miongoni mwa mengine muhimu.

Wamejadili hususan kuhusu harakati zinazoendelea kuelekea kongamano la Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na ahadi za Jamhuri ya Korea.

Katibu Mkuu amerejelea kuelezea kusikitishwa kwake kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) kubadili msimamo wake dakika ya mwisho kuhusu mwaliko wake kwake kuzuru eneo huru la viwanda la Kaesong. Amekariri kuwa hatoacha kamwe kuendeleza juhudi zake za kuunga mkono mazungumzo na maridhiano kati ya Jamhuri ya Korea na DPRK.