Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Ethiopia imepita 200,000

Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini nchini Ethiopia imepita 200,000

Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao wamekimbilia nchini Ethiopia tangu kuzuka kwa mapigano nchini Sudan Kusini katikati ya Disemba mwaka 2013 imepindukia 20,000 huku wakimbizi Zaidi wakitarajiwa  baada ya machafuko mapya mpakani.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wakimbizi hao 199,000 wako jimbo la Magharibi mwa Ethiopia la Gambella , wakati wengine 3,000  wako katika jimbo la jirani la Benishangul-Gumuz .

Wafanyakazi wa UNHCR wameshuhudia miminiko la wakimbizi hao kuanzia 1000 kwa mwezi robo ya kwanza ya mwaka huu hadi kufikia Zaidi ya 4000 kwa mwezi walioandikishwa Aprili. Wakimbizi wapya wanaowasili wanasimulia masahibu ya kutembea kwa siku kadhaa msituni wakiwa na chakula kidogo sana na maji , wakiambatana na mizigo kidogo au bila chocote.

UNHCR imekuwa ikiwahamishia kwenye kambi ya wakimbizi ya Pugnido ambayo kwa sasa inahifadhi karibu wakimbizi 60,000 wa Sudan Kusini na kwenye kambi ya Tierkidi ambayo ina jumla ya wakimbizi  50,000.