Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto hatarini kubeba mzigo wa machafuko Burundi: UNICEF

Watoto hatarini kubeba mzigo wa machafuko Burundi: UNICEF

Watoto wako katika hatari kubwa ya kubeba madhila ya machafuko yanayoendelea mjini Bujumbura nchini Burundi na viunga vyake , amesema mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi Leila Gharagozloo-Pakkala.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNICEF, Christope Boulierac, kumekuwepo ripoti za ukiukwaji wa haki za watoto tangu kuanza kwa maandamano ndani na nje ya mji wa Bujumbura mnamo April 26, ikiwemo :

« Watoto waliojikuta katikati ya maandamano, kuwekwa rumande, kujeruhiwa pamoja na kisa kimoja cha mtoto kuuawa. Jeshi la serikali nchini Burundi linapaswa kuhakikisha watoto hawaingizwi katika maandamano yoyote ambayo yanaweza kuwaweka hatarini hadi kuhatarisha maisha yao. »

Akizungumza za waandishi wa habari mjini Geneva, Bwana Boulierac amesema UNICEF inaendelea kufanya uchunguzi nchini humo ili kubaini ni shule ngapi zimefungwa kwa sababu ya tatizo la usalama na pia kuthibitisha hali iliyopo ndani ya magereza nchini humo.