Ushawishi wa viongozi wa dini kumaliza mizozo ni wa kipekee: Guyo

28 Aprili 2015

Ushawishi walio nao viongozi wa dini kwa wafuasi wao unaweza kutumika kumaliza ukatili, mauaji na mizozo inayoendelea maeneo mbali mbali duniani ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Iraq, Syria na Libya.

Hiyo ni kauli ya Guyo Liban Dadacha mjumbe wa Tume ya Taifa ya uwiano na maridhiano nchini Kenya alihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa huko Fez Morocco.

(Sauti ya Guyo-1)

Mjumbe huyo akagusia vile ambavyo tume ya uwiano na maridhiano nchini  Kenya iliyobuniwa mwaka 2008 imeleta mabadiliko kuhusu kauli za chuki na uchochezi.

(Sauti ya Guyo-2)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter