Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado maelfu ya watu wahitaji msaada Vanuatu: OCHA

Bado maelfu ya watu wahitaji msaada Vanuatu: OCHA

Mwezi mmoja baada ya kimbunga PAM kupita kwenye visiwa vya Vanuatu, operesheni za kibinadamu zinazoongozwa na serikali zinahitaji ufadhili kwa haraka ili kuendelea kutoa usaidizi wa chakula, maji ya kunywa na makazi kwa walioathirika.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, imesema hayo kwenye taarifa iliyotolewa leo, ikieleza kwamba kimbunga kimeharibu zaidi ya asilimia 90 ya mazao, na kuacha raia wanaotegemea kilimo bila chanzo cha kipato.

Kwa mujibu wa OCHA, takriban watu 110,000 hawana huduma ya maji ya kunywa, na bado watu karibu 6,000 wanaishi kwenye makazi ya muda katika maeneo yaliyoathirika zaidi ya Tafea na Shefa.

Hadi leo, ni asilimia 36 tu ya dola milioni 29.9 zilizoombwa, ambazo zimeahidiwa tangu Machi, 24.